Mkuu wa Mkoa wa Kagera ndugu John Mongela aliamua kutembelea wilaya ya Kyerwa na Karagwe mnamo tarehe 29/1/2015 na 31/1/2015.Ziara ya mkuu wa Mkoa ililenga kutembelea miradi ya maji na ujenzi wa maabara wilayani Karagwe na Kyerwa.

Jambo la kufurahisha katika ziara hii ni kwa jinsi maandalizi ya mapokezi ya Mkuu wa Mkoa huyu yalivyowafanya watendaji wengi wa Serikali kujipanga na kuhakikisha zira ya mkuu wa mkoa haitaibua jambo lolote ambalo lingeweza kuwa surprise kwao,Watendaji wengi wa Sekali wilayani Karagwe na Kyerwa hawana tabia ya kuitembelea miradi na kujiua kwa kina na mara nyingi huwa wanapewa taarifa tu jinsi miradi inavyotekelezwa.Lakini wakati Mkuu wa Mkoa alipoahidi kutembelea Wilaya hizi mbili, basi wiki moja kabla ya ujio wake watendaji wakuu wote na kamati mbalimbali walikua wanatembelea mradi  mmoja kwenda mwingine na kuijua kwa kina.

Ofisi yetu ya TAEEs Karagwe pamoja na timu nzima ya TAEEs Karagwe  ilitoa ushirikaiano wa hali ya juu katika kuhakikisha watendaji hawa wa Halmashauri pamoja na kamati mbalimbali wanapata yale waliyokua wanayahitaji kutoka kwetu.